
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanznaia (TBL) Mwanza, Richmond Raymond akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya jinsi kiwanda hicho kilivyoweka utaratibu wa kuwapatia wananchi maji ya bure kutoka kiwandani hapo. Prof. Mwandosya alifanya ziara kiwandani hapo kuona juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya Binadamu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra ya maadhimisho za Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment