Sherehe hizo zinatarajia kufanyika katika ukumbi wa NSSF Waterfront, Dar es Salaam, ambapo zitaambatana na kutangazwa kwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2010.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Ofisi za Shirikisho la Soka nchini TFF, Katibu mkuu wa Taswa Amri Muhando, alisema kuwa kamati ya utendaji ya chama hicho imeteuwa Kamati ya watu 17 ya kusimamia mchakato wa kuwapata washindi hao wa kila mchezo kulingana na vyama vilivyotuma mapendekezo na majina yao na kisha kamati itachagua Mwanamichezo Bora wa Tanzania miongoni mwa washindi hao.
“Kamati hiyo itahusisha watu 15 ambao hawahusiki na TASWA na wawili kutoka TASWA kwa ajili ya kusimamia mchakato huo wa tuzo hizo, ambapo TASWA yenyewe itabaki na jukumu la kuandaa sherehe ya tuzo,”alisema.
Amir, alisema kuwa lengo kubwa la kuunda kamati hiyo ikiwa ni kuwashirikisha kwa pamoja wadau na kuifanya tuzo iliyo bora zaidi.
No comments:
Post a Comment