Hatua hiyo ya TFF imekuja siku chache baada kufanyika Mkutano mkuu wa chama hicho, katika ukumbi wa NSSF Waterfront, ambapo mkutano huo uliwakutanisha wanachama mbalimbali chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Katibu mkuu wa TFF, alisema kuwa mkutano huo ulioanza juzi na kufikia tamati jana ulitoa mapendekezo makuu matatu pamoja na la kamati ndogo.
Mapendekezo hayo ni:-
1:- Kupitisha bajeti ya mwaka 2011 ambayo inaonyesha kuwa matarajio ya makusanyo kutoka vyanzo mbalimbali ni Sh. 6,199,143,120/= na matumizi ya Sh. 6,128,354,040. Kwa mujibu wa bajeti hiyo kunja nakisi ya Sh. 70, 789, 080 ambayo kimahesabu inaonekana kuwa ni ndogo.
Hata hivyo kiwango hicho cha mapato hakitoi picha halisi ya fedha zinazotarajiwa kuingia TFF kutokana na masuala ya kiufundi yanayoendana na fedha za udhamini.
2:- Mkutanomkuu pia uliipa ridhaa kamati ya utendaji kuanza mchakato wa kuongeza wanachama wapya baada ya serikali kutangaza mikoa mipya mine.
Kwa mujibu wa katiba ya TFF, moja ya sifa kuu za kuwa mwanachama wa TFF ni mikoa ya kijiografia ya serikali. Mikoa hiyo mpiya iliyotangazwa na serikali ni Simiyu, Geita, Njombe na Katavi.
3:- Mkutano mkuu pia ulipitisha pendekezo la kamati ya utendaji la kuunda kamati ndogo ya Ligi Kuu ambayo itaundwa kwa lengo la kuendesha Ligi Kuu kwa Uhuru.
Mbali na maamuzi hayo mawili, Mkutano Mkuu pia ulijadili kwa kina mpango wa kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni hadi kufiki watatu, lakini suala hilo likaachwa kwa kamati ya Utendaji kulitengenezea taratibu kabla ya kuanza kutumika msimu wa mwaka 2013/14.
No comments:
Post a Comment