Mwandishi wa habari, Bakari Kimwaga, akiwa mapokezi ya nyumba ya kufikia wageni wakati akisaka vyumba mjini Songea jana usiku baada ya kukataa kwenda kulala katika vyumba vilivyoandaliwa na wenyeji wa ziara ya kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma chini ya Mwenytekiti wake, Zitto Kabwe , kutokana na kuandaliwa nje ya mji njia ya kuelekea Namtumbo Hotel ya Country Side, iliyopo umbali wa zaidi kilometa 2 toka mjiniWaandishi hao, wakiendelea kusaka vyumba usiku huo wakipita katika mitaa ya mjini Songea bila mafanikio, Sasa sijui walilala wapi ama walipewa mikeka???? Siku iliyofuata yaani leo asubuhi walitembelea katika milima yenye madini hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge hesabu za mashirika ya Umma, Zitto Kabwe (wa nne kulia waliosimama ) akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea madini ya lilanga kwa ajili ya kuzalisha chuma yaliyopo kijiji cha Mdindi wilaya ya Ludewa nyuma yao ni mlima wa madini hayo ,kamati hiyo leo ilitembelea eneo hilo la kueleza kusikitishwa na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi huo, aliyechuchumaa chini wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Filikunjombe, ambaye ni mbunge wa jimbo hilo la Ludewa.
No comments:
Post a Comment