Habari za Punde

*WIZARA YA AFYA YAZINDUA PIKIPIKI ZA KUBEBEA WAGONJWA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Haji Mponda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, juu ya mpango wa Serikali kuanzisha ununuzi wa Pikipiki za kubebea wagonjwa ili kuzuia vifo vya wakinamama wajawazito na watoto katika maeneo ya vijijini. Serikali inakusudia kununua Pikipiki 400 ambazo zitasambazwa maeneo mbalimbali hapa nchini. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt Deo Mtasiwa. Picha Zote na Tiganya Vincent-MAELEZO

Waziri wa Afya na Ustawi, Dkt. Haji Mponda (aliye juu ya pikipiki) akizundua Pikipiki maalum iliyotengezwa na Kampuni ya E Ranger ya Afrika Kusini, kwa ajili ya shughuli za kubebea wagonjwa ili kudhibiti vifo vya mama na watoto. Pikipiki hizo kila moja imegharimu Dola za Kimarekani 5,900. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo asubuhi kwenye Ofisi za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa madereva walipata mafunzo ya matumizi ya pikipiki maalum za kubebea wagonjwa, akionyesha jinsi ya kumsafirisha mgonjwa kwa kutumia usafiri huo huku akiwa na muuguzi nyuma.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.