

Waziri wa Nchi ,Ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akizungumza na wafanyabiashara wadogondogo (wamachinga) waliokuwa wakifanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa katika manispaa ya Songea na kusababisha uchafuzi wa mazingira.

Baadhi ya wafanyabiashara wakiitii agizo la Waziri wa Nchi ,Ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (hayupo pichani) la kuwataka kuondoa bidhaa zao katika maeneo ya barabara mjini Songea. Hata hivyo waliutupia lawama uongozi wa manispaa hiyo kwa kuwatoza ushuru kila siku hali iliyosababisha waendelee kufanya biashara katika maeneo hayo.
No comments:
Post a Comment