Habari za Punde

*WAKE WA VIONGOZI WA ZANZIBAR WATOA MSAADA WA NGUO NA VYAKULA KWA WAATHIRIKA WA MABOMU

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Asha Balozi Ally Idd (kushoto) akikabidhi msaada wa khanga kutoka kwa wake wa viongozi, wawakilishi na wabunge wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Zanzibar kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala Leonidas Gama (wa pili kulia). Wanawake hao wametoa msaada huo jana wa vyakula na nguo vikiwa na thamani ya shilingi milioni 6 na laki 8 kwaajili ya waathirika wa mabomu yaliyolipuka hivi karibuni katika kambi la Jeshi la Gongo la Mboto. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Asha Bakari (wa pili kushoto) na Naibu katibu wa (UWT) Salama Aboud (kulia).

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Asha Bakari akieleza jinsi wake wa viongozi, wawakilishi na wabunge wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Zanzibar walivyoguswa na maafa yaliyotokea wakati wa milipuka ya mabomu ya Gongo la mboto na hivyo kuamua kutoa msaada leo wa vyakula na nguo vikiwa na thamani ya shilingi milioni 6 na laki 8 kwaajili ya waathirika wa mabomu hayo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.