Habari za Punde

*WAZIRI NCHIMBI KUFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA TFF LEO

Mutano Mkuu wa mwaka 2010 wa TFF
unaanza leo Machi 26 katika ukumbi wa NSSF
Water Front, Dar es Salaam.
Mkutano huo utakaoanza saa 3 kamili asubuhi utafunguliwa
na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi.
Mkutano huo utakaokuwa na ajenda 16 utamalizika Machi 27
mwaka huu.
Wajumbe wa mkutano huo wameshawasili jijini na kufikia hoteli ya Valentino iliyoko Mtaa wa Aggrey na Spice Inn, Mtaa wa Lumumba.
Ajenda za mkutano ni:-
Kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kusoma na kuthibitisha ajenda, kuthibitisha muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama, kupitisha taarifa za utekelezaji wa Kamati ya Utendaji, kupitisha taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2011, uchaguzi wa nafasi zilizo wazi, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya TFF (kujadili mikoa mipya), kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na wanachama au Kamati ya Utendaji, Mengineyo na Kufunga kikao.
Boniface Wambura
Media Officer TFF


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.