Ofisa Uhusiano wa Benki ya Baclays Tanzania, Moni Msemo, akiendesha mafunzo ya Elimu Fedha kwa watoto Yatima na waishio katika mazingira magumu wanaolelewa katika Kituo cha Friends Of Don Bosco kilichopo Kimara Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipofika kituoni hao leo mchana pamoja na kutoa mafunzo hayo na kukabidhi hundi ya Sh. milioni 3.5 kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi wa shule za Sekondari wanaolelewa na kituo hicho.
Mkurugenzi wa Mkopo Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Musa Kitoi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 3.5 Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Salma Kikwete, Ndahani Mwenda, aliyepokea kwa niaba ya wenzake kwa ajili ya kulipia ada za shule watoto hao Yatima na waishio katika Mazingira magumu, wanaolelewa katika Kituo cha Friends of Don Bosco kilichpo Kimara Dar es Salaam. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo leo chana wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipofika kutoa mafunzo ya Elimu Fedha kwa watoto hao. Viongozi wa Benki ya Barclays, wakisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kituoni hapo leo.
Wasanii ambao ni wanafunzi wanaolelewa katika Kituo cha kulelea Watoto Yatima na wale waishio katika Mazingira magumu cha Friends Of Don Bosco, John Msuha, anayesoma Mwaka wa pili Chuo cha Mzumbe, kutoka (kushoto nyumba yake) ni Aurelia Kiwone, Selina Flujens na Janny Maridadi, wakiimba kutoa burudani wakati wa hafla hiyo.
Mfanyakazi wa benki hiyo, Mchata akiongoza mazoezi ya kujichangamsha wakati wa mafunzo hayo, ambapo vibweka alivyotoa mbele ya wafanyakazi hao vilimwacha hoi kila mmoja ukumbini hapo.
Baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho, ambao pia ni wanafunzi wa Shule mbalimbali, wakiwa katika mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini.
Mtoto Mecky Evansi, akiwaongoza wenzake kucheza ngoma ya Mganda, wakati wa hafla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo, akitoa zawadi ya khanga kwa wanakwaya wa Kituo hicho waliotoa burudani wakati wa hafla hiyo.
Mfanyakazi wa Benki ya Barclays, Mohamed Khatib, akifurahi na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima na waishio katika mazingira magumu cha Friends of Don Bosco, akiwafundisha hesabu.
No comments:
Post a Comment