Na Sufianimafoto Reporter, jijini HITMA ya kuwaombea wanamuziki 13 waliokuwa wa kundi la Five Stars Modern Taarab waliopoteza maisha katika ajali ya gari Machi 21 mwaka huu mkoani Morogoro, itafanyika Aprili 17 kwenye ukumbi wa PTA, Temeke. Akizungumza na Mtandao huu, Katibu wa kamati ya Hitima, Said Mdoe alisema kuwa shughuli hiyo imepangwa kuanza saa 7.00 mchana na maandalizi yake yanaendelea. Mdoe alisema kuwa wadau wote wa sanaa na burudani wanakaribishwa katika kisomo hicho pamoja na kuchangia michango yao. Alisema kuwa michango yako iwasilishwe moja kwa moja kwa mweka hazina (Ashraf Ahmed: 0713232747), au kwa Mwenyekiti (Abbas Mtemvu), Makamu mwenyekiti (Sheikh Omar Alhadi naibu imam wa msikiti wa Kichangani) au Katibu (Said Mdoe, 0713 606109) na utapatiwa stakabadhi. Pia michango hiyo inawezwa kupelekwa ofisini kwake, Kampuni ya Screen Masters iliyopo Kinondoni mtaa wa Togo. Wajumbe wengine wa kamati ni Mhe. Idd Azan (Mbunge wa Kinondoni), Mhe. Azan Zungu (Mbunge wa Ilala), Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf, Naibu mkurugenzi wa TOT Khadija Kopa, Asha Baraka (Mkurugenzi wa Twanga Pepeta), Hadija Shaibu “Dida” kutoka Times FM na Sakina Lioka (Clouds TV) na Mariam Migomba wa TBC. Wajumbe wengine ni pamoja na wakurugenzi wa Five Stars Modern Taarab Hamis Slim, Ali J na Feruz Juma, Mkurugengenzi wa Clouds FM Ruge Mutahaba, Abdallah Feresh (Mkurugenzi Dar Modern Taarab). Alisema kuwa kwa watu wa mikoani wanaweza wakatuma michango yao kupitia M-Pesa kwa namba 0765 111135.
Serikali yamfungulia Mange Kimambi kesi ya uhujumu uchumi
-
Serikali ya Tanzania imemfungulia rasmi mashtaka ya uhujumu uchumi , Mange
Kimambi,Mtanzania anayeishi nchini Marekani.
Taarifa kutoka kwenye tovuti...
2 hours ago

No comments:
Post a Comment