*NI KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI SINGIDA
*PROF. MWANDOSYA AAHIDI KUTEMBELEA MRADI HUO
Na Mwandishi wetu, Dodoma. Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohamed Dewji (MO) leo amembana Naibu Waziri wa Maji Injinia Gerson Lwenge juu ya kukamilika kwa mradi wa maji.
Katika swali lake nyongeza Mh. Dewji amesema tatizo la maji katika Jimbo la Singida Mjini ni kubwa na kwamba wananchi wamekuwa wakihangaika kutafuta maji safi na salama.
Hata hivyo, amesema kuwa kuna mradi wa maji ambao unafadhiliwa na Benki ya BADEA, lakini umechukua muda mrefu kukamilika kwake na kutaka maelezo juu ya hatua zinazochukuliwa. Akijibu swali hilo, Injinia Lwenge amekiri kuwepo kwa mradi huo na kusema kuwa serikali inaendelea kutekeleza ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama. Amesema kuwa mradi huo uko katika hatua nzuri ya kukamilika na kumtaka Mh. Dewji na wananchi wa Singida kuwa subira. Baada ya jibu hilo la serikali, Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya alisimama kuomba kutoa ufafanuzi kuhusu swali la Mh. Dewji, ambapo amesema kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge lijalo, atakwenda kukagua mradi huo.
No comments:
Post a Comment