Habari za Punde

*MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA WA MBEZI MTONI ATUPWA NDANI



*Ni Baada ya kuvunja nyumba za wananchi Kimabavu


*Ashindwa kujitetea mbele ya Mkuu wa Wilaya


*Ageuka Bubu baada ya kushindwa jaribio la kutoroka



MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Mtoni jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Joseph Benjamin, amekamatwa na kuhojiwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Kawe na kasha kutupwa sero.


Jose amekamatwa leo asubuhi baada ya kuunda kikundi cha vijana wa kihuni na kuwaamuru kuvunja nyumba za wananchi wa mtaa huo waliojenga katika eneo la viwanja vilivyogaiwa kwa wananchi baada ya kuwa wazi kwa kipindi kirefu na kuanza kuuzwa kinyemela na Mwenyekiti huyo.


Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo baada ya wananchi hao kukuta nyumba zao zikiwa tayari zimebomolewa na watu wasiojulikana jambo lililowafanya wananchi hao kumuhisi mwenyekiti huyo kutokana na kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu kukodi vijana wa kubomoa nyumba hizo.


Baada ya wananchi hao kukuta tukio hilo walilipoti katika Kituo kidogo cha Polisi Kawe na hatimaye Polisi, Mkuu wa Wilaya, Kamanda Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, wakawasili kwenye eneo la tukio na kumuita Jose ambaye aliyeyusha kufika eneo hilo hadi walipoamua kumfuata eneo la nyumbani kwake.


Walipofika maeneo ya nyumbani kwake walifanikiwa kumkuta Mwenyekiti huyo akiwa eneo la Baa akiendelea kupata kilaji ‘Pombe’ na kuanza kumuhoji huku akijichanganya kwa majibu jambo lililowafanya askari kumsomba pamoja na wajumbe wake na kumpeleka Kituo cha Polisi Kawe na kuwekwa ndani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.