Habari za Punde

*POLIS TEMEKE WAKAMATA WAHALIFU 155 WA MATUKIO MBALIMBALI

POLISI Wilaya ya Temeke imekamata jumla ya wahalifu 155 wa matukio mbalimbali katika msako wao unaoendelea katika walaya hiyo Dar es Salaam ili kupunguza matukio ya wizi uhalifu na ajali.


Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Davisi Misime, kukabiliana na uhalifu na ajali za Barabarani katika Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, wamefanya misako mbalimbali na mikutano 14 ya kuhamasisha Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.

Aidha alisema kuwa baadhi ya maeneo waliyofanikiwa kufanya misako na mikutano hiyo ni Chang’ombe, Kigamboni na Mbagala. Katika matukio ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha/Nguvu, wamefanikiwa kukamata jumla ya watu 11 na kuokota jumla ya risasi 22 za Shotgun Rifle zilizokuwa zimetupwa katika eneo la kutupia takataka Temeke mwisho.

Wahalifu wengine waliokamatwa ni watu 12 katika matukio ya uvunjaji wa nyumba na maduka, ambapo watatu kati yao walikamatwa na vitu walivyoiba muda mfupi tu baada kuvunja nyumba ya mwananchi mmoja huko maeneo ya Mbagala.

Wengine waliokamatwa ni wezi 7 wa magari na Pikipiki, wacheza kamali 6, waliokamatwa na Bangi 19, waliokamatwa wakiwa na kilo 2.2 za bangi na waliokamatwa na madawa ya kulevya ni watuhumiwa 22 waliokuwa na dram 30 za madawa hayo.

Waliokamatwa na Pombe haramu ya Gongo ni jumla ya watuhumiwa 13, waliokutwa na lita 60 za pombe hiyo, wapiga debe 34 na waliokamatwa kwa misako iliyofanywa na Polisi na Polisi wasaidizi wa Halmashauri ya manispaa ya Temeke ni watuhumiwa 31.

Na waliokamatwa kwa tuhuma za kuvunja sheria za Usalama Barabarani, ni jumla ya magari 320 na kutozwa faini ua jumla y ash. 6,400,000 na jumla ya Pikipiki 16 zimekamatwa na kutozwa jumla ya faini ya Sh. 320,000.

Risasi zinazotumika katika Bunduki aina ya Shotgun Rifle zilizotelekezwa katika takataka huko Temeke mwisho. Viafaa vilivyokamatwa muda mfupi baada ya kuibwa katika moja ya nyumba ya mfanyakazi wa Barclays huko maeneo ya Chamanzi jijini Dar es Salaam. Hili ndilo gari lililokamatwa likifanya uhalifu likiwa na vifaa hivyo, ambalo pia kama unavyoliona likiwa halina hata Document yeyote katika kioo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.