Habari za Punde

*YANGA YAMPORA UBINGWA SIMBA KWA TOFAUTI YA GOLI MOJA TU, YANGA BINGWA WA LIGI YA VODACOM TANZANIA BARA 2011

Kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi ya Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu huu 2011, baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza, mchezo ulichezwa kwnye Uwanja wa Kirumba, magoli hayo yakiwekwa kimiani na David Mwape aliyefunga 2 na Nurdin Bakar aliyefunga 1, huku Watani wao wa Jadi Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi yao na Majimaji ya Songea katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imetwaa ubingwa huo kwa tofauti ya kagoli kamoja tu!, na kumvua ubingwa mtani wake wa jadi Simba. Mashabiki wa Yanga, wakitoka uwanjani huku wakishangilia ubingwa wa timu yao baada ya kupata matokeo ya jijini Mwanza huku wakiwashuhudia Simba wakikosa penati ambayo ingewaweka katika upinza na Yanga katika kuamua ubingwa huo kwa njia ya mahesabu.
Warembo wa Vodacom kutoka (kushoto) Idanitha Christopher, Erica Aunt Ezekile, Fadhila Mtamila na Irene Stephen, wakibeba kombe kulirejesha ndani baada ya Simba kushindwa kutetea ubingwa wake kwa kutowafunga mabao mengi Majimaji.
Emaanuel Okwi wa Simba akikosa bao la penati lililozima ndoto za Simba kutwaa ubingwa.
Beki wa Majimaji, Yahaya Shaban, akiondosha hatari langoni kwake, mbele ya Nico Nyagawa (kushoto) na Jerry Santo.
Mohamed Banka wa Simba (kushoto) akichuna kuwania mpira na beki wa Majimaji, Kulwa Mobi, ambaye dakika chache baada ya picha hii alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Jerry Santo.
Warembo wa Vodacom, Erica Aunt (kulia) na Irene Stephen, wakipozi na kombe Uwanjani hapo wakati wakisubiri iwapo Simba itashina bai akabidhiwe kombe hilo.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wa timu yao Mwanza na kushindwa kwa Simba Taifa leo jioni.
Warembo wakipozi na kombe ndani wakati wakisubiri kulitoa nje kwa ajili ya kusubiri Bingwa.
Hii ilikuwa ni shoo ya wasanii wa Vodacom katika kuashiria Ligi hiyo imemalizika kwa usalama chini ya udhamini wa kampuni hiyo ya Vodacom ambayo imeanza kutumia Nembo yake mpya ya rangi nyekundu hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.