Habari za Punde

*BENKI YA KCB YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania, Christine Manyenye akimkabidhi mtoto Beatrice Phinius, wa kituo cha watoto yatima Amani Orphanage Centre cha Boko, sehemu ya msaada wa viloba vya unga wa mahindi na vitu vinginevyo vyote vikiwa na tahamani ya Sh. milioni 1.5, viliyotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya kuwasaidia Yatima na wale waishio katika mazingira magumu wa kituo hicho. Anayeshuhudia nyuma ya watoto ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Margaret Mwegalawa. Christine Manyenye (Kushoto) akiteta jambo na Ofisa Mahusiano kwa Umma wa benki hiyo, Gigi Maajah, baada ya hafla ya kukabidhi msaada kwa Kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre cha Boko jijini Dar es Salaam jana.

Christine Manyenye (kushoto) na mfanyakazi wa benki hiyo tawi la Samora, Shose Kombe, wakifurahi na watoto yatima wanaolelewa na Kituo hicho.


Christine Manyenye (kushoto) akishirikiana na Mkurugenzi wa Kituo hicho Margaret Mwegalawa, kupanga baadhi ya vyakula na vifaa vilivyotolewa kaama msaada na benki hiyo wakati wa hafla iliyofanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya Watoto yatima wa kituo hicho wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa KCB Tanzania Christine Manyenye (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo wenye thamani ya milioni 1.5 kwa watoto 60 wanaolelewa kituoni hapo.Meneja Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Yusuf Shenyagwa, akisaidiana na mfanyakazi mwenzake kushusha viloba vya mchele uliotolewa kuingiza katika kituo hicho.
Sehemu ya msaada uliotolewa kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.