Habari za Punde

*KONGAMANO KUBWA LA G-8 KUFANYIKA NCHINI UFARANSA

Kongamano la G8



Viongozi wa dunia wanatarajiwa kukutana katika eneo Deauville nchini Ufaransa, kwenye kongamano la mataifa manane yenye utajiri mkubwa zaidi duniani G8.

Mkutano wa leo unatokea wakati kumeibuka mataifa mengine ambayo uchumi wake unakua kwa kasi na kuibua hoja ya ushawishi na umuhimu wa G8.


Hata hivyo wadadisi wamesema matuko ya hivi karibuni hususan harakati za mageuzi ya kidemokrasia katika nchi za Kiarabu na changamoto zinazokumba mradi wa nuklia wa Japan yameshinikiza kundi la mataifa hayo makuu kutoa mwelekeo.


Miongoni mwa ajenda ni kiwango cha kuthibiti taarifa zinazosambazwa kupitia mtandao, pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.


Viongozi wa mpito katika nchi za Tunisia na Misri pamoja na Jumuiya ya nchi za Kiarabu wamealikwa ili kujadili mchakato wa kufanikisha utawala wa kidemokrasia katika nchi hizo.


Viongozi wa serikali wa kongamano la G8


Mapema mwaka huu watawala wa muda mrefu katika nchi za Misri na Tunisia waling'olewa madarakani kupitia mapinduzi ya kiraia hali iliyochochea maandamano ya raia kudai mageuzi katika nchi nyingi za Mashariki ya Kati.


Aidha mzozo unaokumba nchi ya Libya unatarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho cha siku mbili.Viongozi hao wamegawanyika huku Urusi ikikosoa vikali harakati za jeshi la NATO dhidi ya majeshi ya Kanali Muammar Gaddafi.


Muungano wa NATO unatekeleza operesheni zake chini ya azimio la Umoja wa Mataifa katika kuwalinda raia wakati wa makabiliano kati ya jeshi la Gaddafi na makundi ya waasi.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.