Wakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mgomo huo leo asubuhi kwenye kituo cha mabasi Ubungo, walisema kuwa wanadai haki yao ya msingi kwa wamiliki wa mabasi wakihitaji kupatiwa miktaba ya ajira na kulipwa mishahara kwa madereva wote.
Aidha walisema kuwa wanahitaji kulipwa mishahara kulingana na kazi wanayoifanya ambayo ni kubwa na ikiwa na dhamana kubwa ya kusafirisha roho za watu kibao, na kutaja kima cha chini wanachohitaji kuwa kisipungue Sh. 350,000 kwa mwezi pamoja na posho za safari.
Na pia wamewataka Polisi wa Usalama wa Mikoa ya Mbeya na Iringa, waache uonevu wa kuwakamata madereva kwa kisingizio cha mwendo kasi, ambapo wamekuwa wakiwaomba rushwa ya Sh. 100,000 hadi 250, 000 ambavyo ni kinyume cha utaratibu.
Pia Madereve hao wamewataka Wamiliki wa mabasi kuwakatia Bima pamoja na kuwekewa akiba ya uzeeni inayotokana na mishahara yao baada ya kukatwa kodi ya Serikali.
Madereva hao walimalizia kwa kuitaka Serikali kuwasimamia ili waweze kupata haki zao na kuiomba Serikali kuongeza muda wa kubadili leseni za udereva na kuvitaka vyuo vya udereva kupunguza Ada ili madereva wengi waweze kujiendeleza na kupata elimu.
Baadhi ya abiria wakiwa katika kituo cha mabasi cha ubungo leo mchana wakiwa wamekwama na safari zao baada ya madereva wa mabasi kugoma.
Baadhi ya madereva na abiria wakiizonga moja ya ofisi iliyopo ndani ya kituo hicho, ambapo abiria waliugonga mlango huo na kuuvunja ili kuwatoa viongozi wa madereva hao waweze kuwapatia suluhishi la safari zao.
Abiria wakiwa bado wameizonga ofisi hiyo, ambapo baadaye walitawanywa kwa virungu eneo hilo na askari Polisi.
Hapa askari wakiwatawanya abiria waliokuwa wakifanya fujo.
Askari wakilinda usalama kituoni hapo.
Askari wakiingia kituoni hapo kwa wingi kuimarisha usalama.
Baadaye baadhi ya mabasi yaliweza kuanza safari.
No comments:
Post a Comment