kwa mujibu wa taarifa za kijasusi, zinasema kuwa kiongozi huyo wa al-qaeda aliuwawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad.
Akitoa taarifa ya kuuawa Rais wa Marekani, Obama amesema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani ilichukua mwili wake.
Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili yakiwamo mashambulizi ya kigaidi katika mjini New York na Washington, iliyotokea mnamo Septemba 11, 2001.
Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al-qaeda, lakini imeelezwa kutanda kwa hofu kuwa huenda wakashambuliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.
Aidha Obama anasema kuwa alitoa taarifa mnamo Agosti mwaka jana, kuhusu mahala alipokuwa amejificha Osama Bin Laden na kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan.
Wiki iliyopita, rais Obama alitoa amri kwa operesheni kufanyika ''kumsaka Bin Laden'' . Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi dogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, Kaskazini mwa Islamabad.
''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema.
***************************************************
Osama bin Laden alizawa mwaka 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia.
Ana zaidi ya ndugu na dada 50.
Baba yake Osama, alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi.
Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa na mavazi ya kifahari na ghali, akiwa likizoni katika miji mbali mbali barani Uropa.
Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themanini aliyapa mgongo maisha haya ya starehe na kitajiri na kujiunga na vugu vugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan.
Na hapo akipigana pamoja na waarabu wenzake, na kuzindua kundi la kigaidi la Al qaeda, mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani.
Kufuatia ghadhabu aliyokuwanayo na Marekani, kwa kuweka majeshi yake katika ardhi ya kiislamu, katika nchi mbali mbali mashariki ya kati.
Osama alioa mke wake wa kwanza akiwa na miaka 17, na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama Bin Laden inaaminiwa kuwa mpka kufariki kwake ameacha jumla ya watoto 17.
No comments:
Post a Comment