Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AMALIZA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO UNGUJA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wahanga kati ya 80, waliopatwa na janga la kuchomewa nyumba zao na watu wasiojulikana eneo la Pwani Mchangani, ambapo hadi sasa idadi kubwa ya watu hao wanaishi katika mahema mawili yaliyojengwa eneo hilo. Dkt Bilal amewahakikishia wahanga hao kuhudumiwa na Serikali ili kuweza kuwa katika usalama zaidi wakati wakisubiri taratibu nyingine kufuatwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Vyumba saba vya Madarasa ya Shule ya Sekondari Nungwi, kakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali mkoa wa Kaskazini Unguja jana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akitoa mkono wa pole kwa Juma Shamte Nyange, ambaye ni baba mzazi wa marehemu, Mole Juma Shamte, aliyekuwa Diwani mstaafu wa Kata ya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, aliyefariki dunia jana katika Kijiji cha Shingwi, wakati Makamu akiwa njiani kuelekea katika shughuli za ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya serikani Mkoani humo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja eneo la Mtowapwani, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali katika mkoa huo jana.







No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.