Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakia Bilal, kuelekea Uwanja wa Eagle Square, kuhudhuria Sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Nigeria, Dkt. Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan, aliyeapishwa leo, jijini Abuja Nigeria.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakia Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mahadhi Juma Maalim kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanaza
wa Rais Zanzibar, Fatuma Fereji, kabla ya kuelekea Uwanja wa Eagle Square, kuhudhuria Sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Nigeria, Dkt. Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan.
wa Rais Zanzibar, Fatuma Fereji, kabla ya kuelekea Uwanja wa Eagle Square, kuhudhuria Sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Nigeria, Dkt. Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan.
*BAADHI YA WASAIDIZI WA VIONGOZI, WAANDIHSI WA HABARI WASOTA WASHINDWA KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA NIGERIA UTARATIBU ZIRO. Huyu ni mmoja kati ya marais walioalikwa kuhudhuria sherehe hizo, akiongozwa na walinzi wa usalama wa Nigeria.
Na Huyu pia akiongozwa kuelekea mahala wanapohitaji wao aelekee.
Na Huyu pia akiongozwa kuelekea mahala wanapohitaji wao aelekee.
Rais wa Liberia, Hellen Johnson Sirleaf, akitoka nje ya Hoteli ya Hilton, kuelekea Katika Uwanja wa Eagle katika sherehehizo.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame (kulia) akiwa ni miongoni mwa waalikwa katika sherehe hiyo, hapa akiteta jambo na baadhi ya viongozi nje ya hoteli ya Hilton, wakati akisubiri kupata utaratibu wa usafiri wa magari.
Hawa ni baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali wakiwa wamekwama bila kujua hatima yao baada ya kuzuiliwa kuingia katika magari kuelekea uwanjani katika sherehe hizo.
"Ai jamani namba nikupige picha!.." Mwanadada huyu aliyejitambulisha kuwa anaishi nchini Uingereza, akimuomba askari huyu wa usalama kumpiga picha ya kumbukumbu baada ya kushangazwa na utaratibu wa Protocal ulivyokuwa ukiendeshwa mahala hapo, kwani ilibidi watu waliokuwapo eneo hilo nje ya Hoteli ya Hilton, kuanz kuchukua picha za kumbukumbu tu baada ya kuona uwezekano wa kufika eneo la tukio haupo japo wamealikwa.
Askari wa usalama wa Nigeria wakibishana wao kwa wao kuhusu utaratibu wa kusafirisha viongozi.
Watu mbalimbali na waandishi wa habari kutoka nchi tofauti wakiomba msaada wa usafiri.
Baadhi ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wakisongamana kuogombea usafiri kuelekea uwanjani.
Angalia picha hii askari wa usalama wakibishana wao kwa wao huku kila mmoja akitaka vile anavyohitaji yeye kuhusu utaratibu wa usafiri.
Eeeeh! ubishani unaendelea.......
Huyu ni miongoni mwa wageni waalikwa akiwa amekata tamaa kabisa ya kuhudhuria sherehe hizo, hapa akiwa nje ya hoteli ya Hilton.
Waandishi wa habari wakiwa wamekata tamaa kabisa ya kupata usafiri wa kuondoka mahala hapo kuelekea uwanjani.
Kinamama hawa wakiwa wamejikatia tamaa wakiondoka mahala hapo kwa masikitiko.
Wanajeshi wakilandalanda katika mitaa ya Nigeria kulinda usalama.
Pikipiki za Askari wa Usalama Barabarani zikiwa tayari kusubiri kuongoza msafara ambao ulikwama na kuchelewa kuondoka nje ya Hoteli ya Hilton.
No comments:
Post a Comment