kazi zao ili kuboresha utendaji wao wa kazi kwani nguvu kazi zaidi itatokana na
vijana hao na siyo vinginevyo.
Wito huo umetolewa leo na Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete wakati akiongea na wanachama wa umoja huo katika ukumbi wa
mikutano uliopo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa hivi sasa vijana wasomi
wanafanya kazi zao na kushindana kwa hoja zenye nguvu kutokana na elimu waliyo
nayo hivyo basi kama wataamua kuwatumia umoja huo utanufaika na kuwa na
mabadiliko ya kiutendaji.
“Shirikianeni na wasomi wa vyuo vikuu,
wafundisheni kazi, wapeni nafasi na siyo kuwapinga kwa kuwaona kuwa wao wanajua
zaidi kuliko ninyi kwani hivi sasa Dunia imebadilika inaenda sambamba na
teknolojia hivyo basi ni rahisi kwa vijana kufahamu mambo mengi tofauti na
wazee na mkumbuke kuwa ili muweze kushindana ni lazima mfanye mageuzi,” alisema
mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete aliwasisitiza kina mama
hao kuwa na tabia ya kutunza siri na kuhifadhi yale yote ambayo yanajadiliwa
ndani ya vikao vya Chama na siyo kuyaongea nje kwa watu wasiohusika.
Mwenyekiti huyo wa WAMA pia aliwataka
wanawake hao kuongeza juhudi ya kuwahamasisha akinamama wengi zaidi kujitokeza
kuwania uongozi katika nafasi za majimbo na kata , kwani ni dhahiri kwamba
wanawake wengi wamejitokeza kwenye nafasi za viti maalum kuliko za kata na
majimbo.
Alimalizia kwa kuwasisitiza kina mama hao
kuongeza ushirikiano kupitia vikundi vya maendeleo ya kiuchumi kwani kwa
kufanya hivyo kutawasaidia wanawake wengi zaidi kufaidika na fursa zilizopo
chini ya mipango ya Serikali ya kumkomboa mwanamke.
Akisoma taarifa ya UWT ya mkoa wa Dodoma
Katibu wa umoja huo Amina Kanyogoto alisema kuwa wamekuwa wakihamasisha
mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kufanya semina kwa kila kata, kutoa
semina kwenye mabaraza ya wilaya na mkoa, kutoa ushauri nasaha kupitia kwa
viongozi wao kujitokeza kwenda kupima kwa hiari na kutoa semia kwa waelimisha
rika.
Aliyataja mafanikio waliyoyapa hadi sasa
ni wanawake wengi kuwa na mwamko wa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
katika ngazi zote baada ya kuhamasishwa na pia kina mama wengi wamekuwa na ari
ya kufanya biashara ndogondogo za kujitafutia kipato cha familia zao.
Kanyogoto alisema, “matatizo
yanayotukabili ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za
uzalishaji mali kwa wajasiriamali wanawake, mikopo inayotolewa haitoshelezi
mahitaji na bidhaa zinazotengenezwa na kina mama bado ni tatizo kwa ajili ya
ukosefu wa masoko na uuzaji wa bidhaa hizo.”
Mama Kikwete yupo mjini Dodoma kwa ajili
ya kuhudhuria matembezi ya uchangishaji wa chakula kwa shule za msingi
yatakayofanika kesho tarehe 29/5/2011 yaliyoandaliwa na Shirika la Chakula
Duniani (WFP) kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa, akisalimia wajumbe wakati wa mkutano. Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment