*****************************
Kutokana na uvumi na matamko mbalimbali kutoka kwa wanachama na baadhi ya wasemaji wa Chadema juu ya waanzilishi wa CCJ. Mimi niliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, napenda kufafanua kama ifuatavyo kuweka wazi jinsi na namna mbalimbali ilivyoabzishwa CCJ, pamoja na wale waliohusika hasa, tofauti na onavyotaka kupotoshwa.
A. KUANZIOSHWA KWA CCJ
Kirefu cha CCJ ni Chama Cha Jamii ambacho kilianzishwa na baadhi ya wananchi wa Tanzania. Chama hiki kilipata usajili wake rasmi wa muda, Machi 2, 2010.
VIONGOZI WAANZILISHI WAIKUWA NI:-
1. Ndugu Richard A. Kiyabo- Mwenyekiti Taifa
2. Ndugu Renatus Muabhi- Katibu Mkuu.
Kutokana na taratibu za usajili wa vyama vya siasa hapa nchini ilibidi tuanze harakati za kutafuta wanachama, tunashukuru kwamba Watanzania wengi walituunga mkono na hata kujiunga na chama chetu, na hatimaye kufikia kupata usajili wa muda, na miongoni mwa watu waliojiunga na chama chetu ni pamoja na Mh. Frederick Mpendazoe.
Mpendazoe alitaka awe Mwenyekiti wetu wa Taifa lakini hatukukubali ombi lake ambalo hakuliwakilisha kimaandishi bali kwa mdomo tu, lakini aliapishwa na chama kuwa msemaji wa CCJ.
Waheshimiwa ambao Mpendazoe anadai walikuwa waanzilishi wa CCJ, hoja hiyo ni ya utata na si ya kweli, maana CCJ haikuwahi kuwa na waanzilishi wa aina hiyo yaani:-
1. Mh. Nape Nnauye , Mh. Harison Mwakyembe, Mh. Samwel Sitta na Mh. Ezekiel Mwabalaswa.
Swali la kumuuliza Mh. Mpendazoe ni je alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa hao aliowataja?, na je wao walikuwa na nyadhifa zipi na kadi namba ngapi za uanachama?, Je amesahau kuwa alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Mh. Sitta kwamba ajiunge na CCJ? hilo atasemaje? Someni gazeti la Mwanachi, ISSN 0856-7573 Namba 03580 la April 6, 2010.
Napenda kuwakumbusha wanasiasa hasa wa Chadema kwamba siasa za udaku hazitawafikisha Ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo Chadema wanajaribu kuonyesha.
Nawakumbusha kwamba Watanzania wamekua kisiasa ndiyo maana hawakuwaingiza Ikulu Chadema kwa kura zao.
Kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kupewa kura kwenye chumba cha kupiga kura, Watanzania wanaelewa kwamba akili za kuambiwa kwenye mkutano changanya na zako kwenye chumba cha kupiga kura.
Nawashauri Mpendazoe na wenzake wa Chadema waache siasa za udaku, Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika si udaku.
Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha.
B. CHADEA NA HARAKATI ZA PEOPLES POWER
Chadema wameonyesha kuwa nguvu ya umma si kura tena, bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani. wao wanajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, ajabu wanayotenda siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa Chama chao ni cha maandamano na vurugu.
Je Wanaiheshimu kweli Demokrasia? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watankwa kzania ura zao sasa kwa nini hawawaheshimu Watanzania?
Wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka Chadema ishinde uchaguzi.
La Hasha! Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao.
Huu ni wakati wa kujengaa taifa letu tukishirikiana na Serikali yetu, na si wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha, Watanzania tuwe makini na Wanasiasa wasio utakia mema utaifa wetu na amani ya nchi yetu.
Tukumbuke kwamba bila amani shughuli za kimaendel eo haziwezikufanyika na hata shughuli zao wenyewe Chadema hawataweza kuzifanya.
Maisha ya wananchi kwa ujumla wake yanategemea amani katika nchi, hivyo sisi Watanzania hatuna budi kulipa kipaumbele suala la amani na maendeleo ya nchi yetu.
Maneno yetu wanasiasa yawe ya kujenga na wala si ya kubomoa amani yetu, na tujifunze kuwa wakweli badala ya kuendekeza siasa za udaku.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Richard A, Kiabo Kada wa Chama Cha Mapinduzi
No comments:
Post a Comment