Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Phil Mwakitawa, alisema ili kuboresha huduma kwa Watanzania, shirika lake limeanzisha mfumo huo kwa lengo la kuhakikisha huduma zinawafikia wateja wao.
"Hii ni huduma mpya itakayowawezesha wateja wa Precision Air kulipia tiketi zao kwa njia ya mtandao wa intaneti," alisema Mwakitawa.
Mwakitawa alisema wateja wa kampuni hiyo kwa sasa watakuwa wanapata huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi ya benki aina ya visa.
"Pamoja na kutolewa huduma hiyo kwa njia ya mtandao, lakini kutakuwa na utaratibu wa kuhakiki kama tiketi iliyotolewa kwa mteja ni mhusika halisi ili kuzuia kujitokeza wadanganyifu na wasio waaminifu," alisema Mwakitawa.
Meneja Masoko wa Precision Air, Emilian Rwejuna alifafanua kwamba kampuni hiyo haikuwa na huduma hiyo awali, hali iliyowachukua muda mrefu wateja wao kupata huduma, lakini mfumo huo mpya utawarahisishia upatikanaji wa huduma.
"Huduma hii ni ya kununua tiketi kwa njia ya intaneti. Sasa wateja wanaotarajia kukata tiketi kupitia intaneti hawatalazimika kwenda ofisi za Precision Air au kwa wakala kulipitia," alisema Rwejuna.
Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho Septemba kuliifanya kampuni hiyo ya ndege kuwa na jumla ya ndege 10, saba kati ya hizo ni mpya. Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.
Kampuni hiyo ya ndege ina mtandao mkubwa wa safari za anga ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara.
Precision Air pia hufanya safari zake za anga katika miji ya Nairobi na Mombasa, Kenya na Entebbe, Uganda.
No comments:
Post a Comment