Habari za Punde

*FLAVIANA MATATA AWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE NA RUSSEL SIMMONS

MAHOJIANO LIVE NA MO BLOG

MO BLOG : Flaviana Matata ni Nani na unamuelezeaje..??

FM :- Naitwa Flaviana Matata Former Miss Universe Tanzania and I am now an International Model based in New York and Europe. Mimi kama Flaviana Matata nikisema niji-describe naweza kusema I am simple but class woman.

MO BLOG :- Nini kilikuvutia mpaka ukaingia kwenye maswala ya Urembo na Uanamitindo..??

FM :- Kiukweli mimi sikuwepo kabisa katika masuala ya urembo wala uanamitindo, lakini I have a friend or a brother called Ruge Mutahaba, wakati nilikuwa nasubiri majibu, yaani nilikuwa nimemaliza college sasa nasubiri matokeo ili nijue what is my next step, akaniambia kuna shindano la Miss Universe, aahh ilikuwa ngumu sana, sana kwangu nikamwambia I can’t do it.

Uunajua nilikuwa Tomboy kwa hiyo nikaona mambo ya urembo, mambo ya kike mi siwezi ukizingatia nilikuwa sijawahi kupaka make-up before na mengineyo. Akaniambia Flaviana you can do it..go…go!! akaniburuta japo nilikuwa sitaki kwenda, lakini nikaenda kambini, nikakutana na wasichana, watu ambao nimeshiriki nao wanajua kuwa sikuwa serious kabisa, nikawa nakula chakula kizuri nakaa Five Star Hotel lakini mwishoni mimi ndio nikashinda, niliposhinda ndio nikagundua Ohoo kumbe I can.!!

Ikabidi niwe serious, hata hivyo nikawa na muda mfupi sana wa kujiandaa kwenda kwenye mashindano, nikaenda na namshukuru Mungu I did well, sio vizuri sana lakini nashukuru Mungu nikawa namba 6 world wide ambayo ni first one in Afrika.

Nilipomaliza hapo nikarudi nyumbani nikawa nasafiri sehemu tofauti tofauti kutokana na kazi za taji nililokuwa nalo, na nilivyovua crown mwaka 2008 mwishoni nikapata contract South Africa, nikaenda huko kwa mwaka mmoja yaani 2009 yote na 2010 kidogo then nikiwa Marekani kwenye mambo yangu ya charity work nikakutana na Russel Simmons akanisaidia ndio nikasaini contract na management ambayo ndio niko nayo Marekani na Europe. Yaah…the rest is history na namshukuru Mungu kwa kweli kwa mpaka hapa nilipo, lakini mtu akifikiria, ndio nilikuwa nawajua wanamitindo, nilikuwa napenda kuwaona lakini mimi I was’nt plan kuwa mwanamitindo.

Kusoma Mahojiano yote ingia hapa http://mohammeddewji.com/blog/?p=8878




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.