Habari za Punde

*KAMPUNI YA ULINZI YA KIWANGO YAJIPANGA KUDHIBITI WIZI WA BETRI ZA MINARA YA SIMU

Na Frank Balile,jijini
KAMPUNI ya Ulinzi ya Kiwango imeweka mikakati ya kudhibiti wizi wa betri za minara ya simu kwa kutangaza zawadi kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wezi hao.

Mpango huo ni kwa ajili ya kuondoa matatizo ya mawasiliano ambayo watumiaji wa simu wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kukosa mawasiliano yanayosababishwa na kuibwa kwa betri hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Utawala wa kampuni hiyo, Bw. Msafiri Pesa, alisema vitenmdo vya wizi wa betri hizo vimekithili sana, hasa Dar es Salaam.
Alisema baada ya kugundua uharifu huo, kampuni yao imeamua kushirikiana na wananchi kudhibiti wizi huo.

“Wizi wa betri hizi unasababisha hasara kubwa kwa kamopuni husika na sisi tuliopewa dhamana ya kulinda, ndiyo maana tumebuni njia hii ili tuweze kudhibiti ama kupunguza vitendo hivi,” alisema.
Bw. Pesa alisema kampuni yao itatoa zawadi ya fedha taslimu sh. 500,000, kwa mtu atakayetoa taarifa za wizi wa betri hizo na kuwa siri kati ya mtoa habari na kampuni.

Alisema kwa Yule atakayesaidia kupatikana kwa betri hizo, atazawadiwa fedha taslimu sh. 250,000 na kuwqa siri kati yake na kampuni.
Alisema kuwa, kwa wananchi ambao watakuwa na taarifa za wizi wa betri hizo, wanatakiwa kuwasiliana na kampuni ya Kiwango kwa kutumia namba za simu, 0715 123444, 0714 882003 na 0655 900321.
“Huu mpango tuliouweka utakuwa siri kati ya mtoa taarifa, atakayetuonesha na kampuni, ni kwa usalama zaidi, hivyo wananchi wasiwe na hofu,” alisema.

Meneja Utawala huyo alisema kuwa, kampunmi yao ipo tayari kushirikiana na makampuni mengine ya ulinzi yanayojishughulisha na ulinzi wa minara ya simu kudhibiti wizi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.