Habari za Punde

*MBOWE CHINI YA ULINZI HADI MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI ARUSHA KUJIBU SHITAKA KESHO

Na Mwandishi Wetu, Jijini

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Dar es salaam jana na kesho anatarajia kusafirishwa hadi Mahakama ya hakimu mkazi Arusha kujbu mashitaka yanayomkabiri.

Kukamatwa kwake kumekuja kufuatia agizo la pili la Hakimu wa Mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya kusanyiko lisilo halali mkoani Arusha Januari 5, mwaka huu.

Akitoa hukumu dhidi ya washtakiwa wengine waliojisalimisha mahakamani baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo Mei 27, 2011, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa, alisema kitendo cha mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo kushindwa kujisalimisha labda anataka kukamatwa na Polisi.

Mahakama hiyo awali iliamuru Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wabunge wawili wa chama hicho, Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini), Josephine Mushumbusi, Richard Mtui, Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Pamoja na washtakiwa hao na wadhamini wao kutofika mahakamani, na Mawakili wao, Method Kimomogolo na Albert Msando, pia hawakutokea mahakamani hapo wakati hati hiyo inatolewa, lakini washtakiwa Joseph Selasini (Mbunge wa Rombo) na Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani siku hiyo, na mahakama haikutoa hati ya kuwakamata kwa sababu wadhamini wao walikuwapo.

Washtakiwa waliohudhuria mahakamani hapo siku hiyo ni pamoja na Nai Steven, Mathias Valerian, John Materu, Daniel Titus, Juma Samuel, Walter Mushi, Peter Marua na Erick Makona.

Hakimu Magesa alisema mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamatwa au kujisalimisha mahakamani hakufanya hivyo wala mdhamini wake, hivyo Ofisa Inchaji wa Polisi anatakiwa kumkamata kwani ni wajibu wake kutekeleza amri halali ya mahakama na si vinginevyo,

“Wote walipewa masharti ya kufika mahakamani kama ulivyo utaratibu na iwapo watakuwa na udhuru wa kibinadamu basi ni wajibu wa wadhamini wao kuhakikisha wanafika mahakamani kueleza kilichowasibu.

Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa, hivyo Ofisa Inchaji amkamate na kufikishwa mahakamani.”

Baada ya kukamatwa Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, Freeman Mbowe, anatarajia kusafirishwa kwenda mkoani Arusha kesho kusomewa shitaka linalomkabiri.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.