Habari za Punde

*KUTOKA CONGO BRAZZAVILLE

Hapa ni geti la kuingilia katika Kivuko cha kusafiria kuelekea Congo Kinshasa, kama ambavyo uanaona Kivuko cha Kigamboni Dar es Salaam, alkini hapa tofauti ni kwamba unapotaka kuvuka kuelekea Kinshasa ni lazima uwe na Passport na igongwe Viza ya kutoka na Brazzaville na kuingia, ila mazingira hayaiendani na shughuli hiyo kiukweli.
Hili ndilo Daraja la kuvukia kuingia katika kivuko, hapa usipokuwa makini utachafua nguo zako kutokana na mabomba ya pembeni jinsi yalivyo na kutu na pia usipikuwa mwangalifu unaweza kuteleza kama unavyoona hapa ni Mama Zakia Bilal, akiwa katika uangalifu mkubwa kuepuka hayo wakati akiwa eneo hilo kwa ajili ya kuvuka.
Hili ni moja kati ya Boti zinazofanya kazi ya kuvusha abiria kutoka Ng'ambo ya Congo Kinshasa na Congo Brazzaville.
Huu ndiyo Ukumbi wa Bunge wa Congo Brazzaville.
Huyu ni mmoja kati ya askari wa Usalama Barabarani wanaoendesha pikipiki za kuongoza Viongozi Barabarani, hapa akijiandaa kuongoza msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kuelekea Uwanja wa Ndege.
Nchi hii kila kona ni ulinzi wa askari Jeshi wanawake na wanaume, pichai ni mmoja wa askari wa kike akiwa na silaha akilinda na kublok magari yasiingilie msafara.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.