Habari za Punde

*TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA KUTOTUMIA TUMBAKU DUNIANI WILAYANI BAGAMOYO

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Hadji Mponda, akizungumza na wananchi wa wilaya ya Bagamoyo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia Tumbaku duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Majengo Bagamoyo. Pamoja na mambo mengine amesema serikali imeandaa mpango mkakati wa miaka 5 kwa lengo la kudhibiti matumizi bidhaa za tumbaku nchini.

· Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (kulia) akipata maelezo kutoka kwa, Rutgard Kagaruki mmoja wa wahamasishaji walio katika mapambano dhidi ya matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini kutoka asasi ya kiraia inayopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku nchini (Tanzania Tobacco Control Forum) wakati alipotembelea banda la maonyesho la asasi hiyo wilayani Bagamoyo leo.

Wanafunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASuBA) wakiwasilisha ujumbe unaopiga vita matumizi ya bidhaa za tumbaku wakati wa maadhimisho ya Siku ya kutotumia tumbaku Duniani leo wilayani

Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.