SHINDANO la kumaka Vodacom Miss Mbeya 2011, linatarajiwa kufanyika Juni 4 mwaka huu katika uwanja wa Sokoine uliopo jijini humo ambapo mshindi wa shindano hili anatarajia kujipatia zawadi ya kitita cha Sh. milioni 1.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo kupitia kituo cha Fred Herbert alisema jana kuwa shindano hilo litashirikisha warembo 13 waliopatikana kupitia mashindano yaliyofanyika katika wilaya za Mbeya na Mbeya vijijini pamoja na Vyuo vikuu.
Aliwataja washiriki kutoka Vyuo vikuu kuwa ni Grace Ngala(20),Shadia Henry(22),Judith Baligenge(22) na Lilian Wilbroad(20).
Kutoka Mbeya vijijini wamo Joyce Malima(20),Mectiy Mbegeze(19) na Fortunate Ande(22) huku kutoka Mbeya jiji wakiwemo Irene Kimaro(19),Sophia Romanus(20),Anna Kiwambo(20),Princes Charles(19),Nunu Hassan(22) na Martha Moses(19).
Hata hivyo Herbert alitaja changamoto ya wadhamini kutojitokeza kudhamini mashindano hayo katika ngazi za wilaya kuwa kikwazo cha kuwapa washiriki kutoa wilaya zote za mkoa wa Mbeya hali inayodhoofisha msisimko wa mashindano kwa kuonekana ya wilaya chache na si mkoa.
Alisema sababu ya kufanyia mashindano katika uwanja wa sokoine ni kumbi ambazo zimekuwa zikitumika kuwa ndogo ikilinganishwa na idadi ya watu ambao hufika kushuhudia.
“Uzoefu tulionao unaonyesha kumbi zetu ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya watazamaji wa shindano sasa tumeona uwanja wa Sokoine unafaa na ndiyo maana tukaamua kufanyia hapo.Sababu ya pili ni watazamaji wapate burudani nyingi na kwa kujinafasi zaidi ukichukulia tutakuwa na Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa” alisema
MAHAFALI YA 16 KIDATO CHA NNE KOM SEKONDARY YAFANYIKA
-
Wahitimu wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom
wakipokea keki kwa niaba ya wahitimu wengine.
Wahitimu wa kidato cha nne 2024 s...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment