Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SONGEA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kusini, Metson Mwakanyamale (kushoto) kuhusu ufugaji wa Mamba, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mazingira DunianiMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Ruvuma, Methord John, kuhusu uzalishaji wa matofali yanayochomwa kwa kutumia Makaa yam awe, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani zilizoanza mjini Songea mkoa wa Ruvuma, kwenye Uwanja wa Majimaji.


Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya za Songea baada ya kuwasili mjini Songea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Moa wa Ruvuma.
Ngoma ya asili ya makaribisho ya Makamu wa Rais kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akifurahia ngoma ya asili baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa mjini Songea.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.