Habari za Punde

*TASWIRA KATIKA PICHA

Hii ni picha iliyopigwa kwa juu ikionyesha sehemu ya mandhali murua ya Jiji la Dar es Salaam, lakini mambo yanayotokea ndani ya jiji hili mengine huwezi kuamini, eti wakazi wa jiji hili wameshindwa kabisa kuwa na utaratibu wa kutunza mazingira na kudumisha usafi, kiasi kwamba wengine wakiwa katika daladala wanaweza kunywa maji na kisha akatupa tu chupa hovyo popote tena bila kuona aibu wala kujali ni mahala gani anatupa chupa hiyo. Eti jiji kama hili limeshindwa na mji mdogo kama wa Moshi ambao umekuwa na utaratibu na mpango madhubuti wa kutunza mazingira na kusimamia usafi, lakini hii imetokana na msimamo wa dhati katika kuhakikisha suala zima la usafi kiasi kwamba mtu anayetoka jiji la Dar es Salaam, anapoingia Moshi huona hata aibu kudondosha hata kijivocha alichoisha kwangua kwani pindi utakapoonekana kutupa hata kipisi cha sigara utatozwa faini tena kubwa isiyolingana na ulichotupa hii ndiyo inayowafanya watu wakaheshimu mazingira sasa iweje jiji la Dar inashindikana nini???? Ninaimani ukiwapo usimamizi madhubuti hakuna litakaloshindikana, tukiamua tunaweza "YES WE CAN". Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
Yale yaleeee!!!!!!, Kamera iliwanasa wafanyakazi hawa wakifanya usafi wa kuzibua mtaro wa maji machafu maeneo ya Victoria Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, wilayani Kinondoni -Dar es salaam. Hivi karibuni Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni ilibukana kaulimbiu yake isemayo ( KINONDONI SASA UCHAFU BASI ! ) Je! kweli katika mazingira kama haya maudhui ya msemo huo kweli itawezekana?? . Na hii imetokana na kuwa wakazi wa Jiji hili hawana elimu ya kutosha kuhusu utunzaji wa mazingira na kutokuwa na msimamo wa kusimamia usafi wa mazingira tena kuanzia katika ngazi ya Mtaa, sidhani kama ikitungwa sheria ya kumtoza faini na kumfikisha Mahamani kila atakayekutwa akitupa taka hovyo na bado ukakuta taka zimezagaa katika mitaa. Mtaro kama huu si kwamba umejaa maji kwa sababu ni mengi la hasha ni kutokana na wakazi wa jiji hili waliowengi wamekuwa na mazoea ya kutupa taka katika mitaro tena nyakati za usiku.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.