Habari za Punde

*WANAFUNZI 31 WENYE ULEMAVU WAHITIMU MAFUNZO YA UPISHI

Mkurugenzi wa CEFA Tanzania, Dario De Nicola (katikati) akiwahutubia wanafunzi waliohitimu katika taasisi yake ya CEFA hawapo pichani katika mahafali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.(kushoto) ni Mwalimu wa mapishi.
katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi
31 wenye ulemavu walihitimu mafunzo na kupata vyeti katika programu hiyo tayari jumla ya wanafunzi 5 wa mambo ya upishi wamepata ajira katika hoteli mbalimbali za kitalalii nchini.
Mkurugenzi wa CEFA Tanzania Dario De Nicola akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo cha mapishi mmoja wa wahitimu katika mahafali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, wapili (kushoto) ni Ofisa Mipango wa Umoja wa Ulaya nchini, Paddy Siyanga na Meneja Miradi wa Rader Devolopment Diana Makumba.
Ofisa Mipango wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania Paddy Siyanga (kulia)akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uselemala (Carpentry Course) Hamida Chande ambaye ni miongoni mwa wanafunzi 31 wenye ulemavu waliohitimu mafunzo katika Taasisi isiyo ya kiserikali ya CEFA ya jijini Dar es Salaam.
Kozi zinazotolewa kwa walemavu hao ni pamoja na Uokaji wa mikate, (Bookery and Housekeeping) na useremala ambapo taasisi ya Cefa imeshilikiana na RADER ,CCRDB kwa msaada wa Umoja wa Ulaya (EU). Picha na Albert Jackson.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.