Habari za Punde

*VODACOM 'KUWAPAGAWISHA' WABUNGE IJUMAA HII


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Ijuma hii itajumuika pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla ya chakula cha usiku pamoja na burudani ya muziki katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,  Mwamvita Makamba, chakula hicho ni sehemu ya utamaduni wa kampuni hiyo wa kuimarisha mahusiano na wadau wake mbalimbali ikiwemo Bunge na Serikali pamoja na kutambua juhudi za wadau hao katika maendeleo ya taifa na watu wake.

"Tumekuwa na utamaduni wa kuandaa hafla za aina hii wakati wa Bunge ila ya mwaka huu mambo yatakuwa mazuri na ya aina yake ikilinganishwa na tulizowahi kufanya miaka ya nyuma na kwa mantiki hiyo kauli mbiu ya mwaka huu ni "More Than Ever Before"  na tunamaanisha"Alisema Mwamvita.

"Vodacom Tanzania inakwenda Bungeni mjini Dodoma ikiwa na sura mpya kufuatia mabadiliko makubwa katika muonekanao wake wa rangi na kauli mbiu ambayo sasa ni  "kazi ni kwako" na hivyo tunataka kuwadhihirishia waheshimiwa wabunge upya wetu katika kila jambo tunalolifanya si tu katika utoaji wa huduma za mawasiliano ya mkononi nchini"aliongeza Mwamvita

Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda anatarajiwa kuongoza hafla hiyo itakayohudhuriwa pia na Spika wa Bunge Mama Anne Makinda, Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe pamoja na wabunge wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri watakaojumuika na viongozi wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Dietlof Mare.

Mwamvita alisema anatambua kuwa wabunge kwa sasa wapo katika kazi nzito ya kujadili bajeti ya Serikali kazi ambayo Vodacom inaitambua na kuiheshimu na hivyo pamoja na mambo mengine bado suala la kuwaandalia hafla za aina hiyo nalo lina sehemu yake ili kuwapatia fursa ya kukutana nje ya mazingira ya kazi.

"Kwa niaba ya Uongozi wa Vodacom na wafanyakazi wake napenda kutumia fursa hii kwa heshima na taadhima kuwakaribisha waheshimiwa wabunge wote kujumuika pamoka katika usiku wa Vodacom na Bunge utakaoburudishwa na Mwanamuziki Banana Zorro, Diamond pamoja na Bi.
Shakira ikiwa ni kuendeleza mahusiano mema yaliyopo yenye azma ya kujenga taifa lenye maendeleo makubwa katika nyanja ya mawasiliano ya simu za mkononi."alisema

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.