· * Wanakijiji wamtaka ahame, Polisi yaingilia kati
KIKONGWE mwenye umri wa miaka 85, mkazi wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la, Sadiki Salehe, amejitia matatani baada ya kulala na maiti ya mtoto wake pekee kwa siku sita.
Habari za kuaminika kutoka kijijini hapo, zimesema kuwa wakati harufu hiyo ikiendelea kuzagaa eneo la nyumba yake na majirani, Kikongwe huyo alikuwa akiendelea kuandaa futari karibu na mlango wa chumba cha marehemu.
KIKONGWE mwenye umri wa miaka 85, mkazi wa Ilolo kata ya Ruanda Jijini Mbeya aliyefahamika kwa jina la, Sadiki Salehe, amejitia matatani baada ya kulala na maiti ya mtoto wake pekee kwa siku sita.
Habari za kuaminika kutoka kijijini hapo, zimesema kuwa wakati harufu hiyo ikiendelea kuzagaa eneo la nyumba yake na majirani, Kikongwe huyo alikuwa akiendelea kuandaa futari karibu na mlango wa chumba cha marehemu.
Mtoto wa kikongwe huyo alijulikana kwa jina la Salehe Sadiki (38) kwa mara ya mwisho alionekana Jumatano ya wiki liliyopita (Agosti 17, 2011).
Kikongwe huyo alipohojiwa alisema kuwa Jumatano ya Agosti 24 mwaka huu akiwa nyumbani kwake alikuwa anahitaji dishi la kuogea ambalo lilikuwa katika chumba cha marehemu ambaye alikuwa akiishi nje ya nyumba inayotizamana na ya baba yake umbali wa meta 3.
Harufu hiyo ilimshtua kikongwe huyo ambaye aliamua kwenda msikiti wa Soweto uliopo Jijini Mbeya kwa Imamu, Eliasa Selemani, ambaye naye alimtaarifu balozi wa mtaa huo Iddi Malole kuhusu tukio hilo.
Imamu Eliasa na Balozi Malole kwa pamoja walimtaarifu Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Benson Mbwana, kuhusu tukio hilo la kushangaza ambaye alimua kutoa taarifa kituo cha Polisi Mwanjelwa.
Kituo cha Polisi cha Mwanjelwa kilishindwa kushughulikia suala hilo ambalo lilipelekwa katika kituo cha Polisi cha Kati (CENTRAL POLICE) ambacho kiliruhusu kuzikwa kwa mwili huo ambao ulikuwa umeharibika vibaya kwa kupasuka huku Polisi ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Baada ya tukio hilo baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walisikika wakisema kuwa tukio kama hilo kwa Kikongwe huyo si mara ya kwanza kumtokea mzee huyo ambaye hapo awali alidaiwa kumuua mkewe na kumweka uvunguni mwa kitanda kwa zaidi ya siku nne hali iliyomfanya atumikie kifungo cha zaidi ya miaka 8 jela kutokana sakata hilo.
Polisi walipoona hayo ilimuondoa mzee huyo eneo la tukio kwa nguvu ili kunusuru maisha yake.
Wakati polisi ikiondoka na mzee huyo wakazi hao walisikika wakiwaka “Hatumuhitaji huyu Mzee katika makazi yetu na asirudi tena kijijini kwetu kutokana na vitendo hivyo licha ya sura yake ya upole aliyonayo na kushinda msikitini”.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho wakiwa nyumbani kwa Kikingwe huyo.
Waumuni wa Dini ya Kiislamu wakimswalia maiti huyo kabla ya kuelekea mazikoni.
No comments:
Post a Comment