Habari za Punde

*MOE DEWJI APELEKA MRADI WA MAJI WA BILIONI 20 SINGIDA


"Mangumbaru wa siasa wananichafua" Dewji

* Apeleka Singida mradi wa maji wa bil 20/-
Na Mwandishi Wetu
 

 MBUNGE wa Singida Mjini, Mohammed Dewji amesema mangumbaru
 (watu wenye machachari, matata na fujo) wa siasa
 wanamchafua, kwa lengo la kuchukua kiti chake cha ubunge.
 
 Dewji, maarufu kwa jina la Mo, ametoa kauli hiyo wakati
 akifanuzi tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu waliodai ni
 wakazi wa Singida, walioda eti kwamba hajafanya chochote cha
 maendeleo katika jimbo lake tangu achaguliwe kuwa mbunge.
 
 Tuhuma na malalamiko hayo yaliyotolewa na baadhi ya watu
 waliodai ni wananchi wa Singida kupitia mtandao wa Facebook,
 wakati wa kubadilishana mawazo na mbunge huyo.
 
 Pia Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema)
 aliwataka wana-Singida kuungana na Watanzania wengine
 kufanya maandamano kudai ahadi ya maisha bora kwa wote kama
ilivyoahidiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 iliyoko madarakani.

 Lema akiwa na wabunge wenzake, Chiku Abwao na Regia Mtema
 (Chadema - Viti Maalumu), alisema hayo wiki hii mjini
 Singida kwenye mkutano wa hadhara, huku akidai umefika
 wakati kwa wananchi wa Mkoa wa Singida ambao ni ngome ya
 CCM, kukiondoa chama hicho madarakani.

Katika michango yao kwenye Facebook, wananchi hao
 walioruhusiwa kutoa maoni na dukuduku zao kwa Dewji, walidai
 kutoona maendeleo yoyote katika jimbo hilo kwa madai kwamba
 wananchi wa Singida wamekuwa wakiteseka na maisha kwa kukosa
maji, ajira na masuala ya maendeleo.

Katika ufafanuzi wake kuhusu malalamiko hayo, Dewji alisema
tangu kuchaguliwa kwake amekuwa mstari wa mbele kuleta
 mabadiliko ya kimaendeleo kwenye maeneo ya kero za maji.

 Dewji alisema amefanikisha uchimbaji wa visima virefu zaidi
 ya 21 kwenye kata za Unyambwa, Mungu Maji, Unyamikumbi,
Mwankoko, Mtamaa, Mandewa na Mtipa pamoja na baadhi ya kata
 za Mjini kama Kindai, Mitunduruni na Utemini.

 Dewji pia aliongeza kuwa bado anaendelea na jitihada za
 kukabiliana na tatizo hilo kwa kuibana Serikali itekeleze
 mradi mkubwa wa Benki ya Dunia wa kuchimba visima 10 jimboni
 na anaendelea kuibana Serikali ifanye haraka kumalizia mradi
 mkubwa mwingine wa maji unaofadhiliwa na Benki ya BADEA na
 OPEC.

 "Mradi huo ukikamilika ndio utakuwa ufumbuzi wa tatizo la
 maji Manispaa ya Singida... Mradi huu utabadilisha
 miundombinu yote ya maji safi ndani ya manispaa yetu.
 Unatarajia kukamilika mwaka 2013 na utagharimu takriban sh.
 bilioni 20," alisema Dewji.

 Kuhusu ajira, Dewji alieleza kuwa amekuwa mstari wa mbele
 kutoa Ajira kwa vijana kupitia kampuni yake ya Mohamed
 Enterprises Limited (MeTL) sambamba na kampuni nyingine
 mbalimbali.

Alifafanua zaidi kuwa yuko mbioni kuwekeza katika jimbo
lake kwa kufungua kiwanda kitakachotoa fursa zaidi kwa
 vijana na wakazi wa Singida kujipatia maendeleo na ajira, na
 kwamba kwa sasa anaendelea kuwasiliana na wataalamu
 mbalimbali wa uwekezaji ili kuona kama kuna fursa za
 kuwekeza katika manispaa ya hiyo.

 Alipongeza kupokelewa kwa mwito wa kuhamasisha michezo
 katika jimbo lake na kusisitiza kuwa ataendelea kunyanyua na
 kuibua vipaji kupitia mashindano yake yajulikanayo kama
 Mohammed Dewji Cup yakiwa na takriban miaka saba na yamekuwa
 na mafanikio makubwa kwa vijana wazaliwa wa Singida.

"Kuhusiana na suala la ujenzi wa Uwanja wa Namfua,
nilishaanza ukarabati katika eneo la jukwaa kuu, wananchi ni
 mashahidi... kama wanaufahamu uwanja ulivyokuwa mwanzo na
 wakati wa mashindano ya riadha kitaifa, nilikarabati eneo la
kukimbilia wanariadha.

 "... Bado nitaendelea kukarabati kwa awamu mpaka
tutakapoukamilisha. Ukumbuke ahadi hii haikuwa yangu peke
> yangu. Lakini nimeshanunua nyasi za bandia ambazo
 zimenigharimu sh. milioni 250... Natarajia kuziweka hizo
 nyasi mwaka 2012/2013," alisema Dewji.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.