Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AJUMUIKA NA WANANCHI SWALA YA EID EL-FITR MNAZI MMOJA DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum, wajumuika pamoja na waumini wa dini ya kiislamu kuswali swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa pili kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (kulia), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba (kushoto), wakiwa katika swala ya Eid El-Fitr, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Immam Mkuu wa Msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam, Masoud Mohamed Jongo,  akitoa mawaidha baada ya swala ya Eid El-Fitr iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Swala ya Eid El-Fitr.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El- Fitr.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Ibrahim Lipumba, baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El-Fit.
 Watoto nao hawakuwa nyuma katika kuhudhulia swala ya Eid, hapa wakiingia katika Viwanja vya Mnazi mmoja asubuhi kujiandaa na swala hiyo.
Hawa ni sehemu tu ya kinamama waliohudhulia swala hiyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.