Baadhi ya wageni waalikwa wakipata futari katika hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Ubalozi wa Tanzania Hapa London Leo uliwaalika watanzania wote kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu kwa watanzania wote. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa na vilipikwa katika hadhi ya kitanzania.
Naibu Balozi Mh Chabaka aliwashuru wadau wote ambao waliweza kuja na kujumuika na kufuturu kwa pamoja.
Aidha, Balozi aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi katika hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili yetu hivyo tuutumie ipasavyo.
Mtoto wa mwanamuziki maarufu nchini Tanzania ambaye ni marehemu kwa sasa, Remmy Ongala, Aziza Ongala, akila pozi na Frank wakati wa hafla hiyo.
Ofisa wa Ubalozi wa Tanzanjia nchinii Uingereza, Carol, (kushoto) akila pozi na Jestina George.
Freddy Macha katikati akiwa na wadau.
Wageni waalikwa ambao wengi wao wakiwa ni wabongo wakipata Futar.
Watoto pia walikuwapo wakijivinjali na futari murua.
Mzee Kiondo kutoka Ubalozini akisubiria Futari.
Ustadhi akiangalia muda ili kuweza kutoa adhana watu waweze kupata ibada na baadaye futari.
Wadau wakipata futari...
Wageni waalikwa wakiomba dua baada ya futari...
Kina Mama pia walikuwapo hapa ulifika muda wao wa kujisevia..
No comments:
Post a Comment