Habari za Punde

*BONGO MOVIE HOI KWA WAZEE WA LEADERS CLUB

Na Mwandishi wetu
TIMU ya Leaders Club imeisambaratisha timu ya Bongo Movie bao 1-0  katika mchezo maalum wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kutokana na wachezaji wote kuonyesha viwango vya hali ya juu.
Leaders Club ikiongozwa na Doyi Moke,  Adam Sapi, Christopher Semi, Baraka, Makoye, Juma Pinto, Idd Janguo, Abdul Tall, Michael, Kibwana Matephone na Charles Nyarusi walitawala mchezo huo ambao ulivuta mashabiki wengi kutoka kona mbali mbali za jiji.
Bongo Movie iliongozwa na Jacob Steve, (JB), Masoud Bitebo, Steven Nyerere na Vincent Kigosi ‘Ray’ ilishindwa kumudu kasi ya timu ya Leaders.
Baada ya kosa kosa nyingi, Leaders Club ilipachika bao la ushindi kupitia kwa Juma Tall kufutia ushirikiano mzuri na Adam Sapi na Juma Pinto.
Bao hilo liliwachangaya zaidi Bongo Movie ambao walipoteza ‘network’ uwanjani na kuanza kumvamia mwamuzi kila wakati wanapocheza faulo.
Tofauti na mchezo wa soka, mchezo huo ulionekana kuwa wa upande mmoja zaidi kutokana na uwezo mkubwa wa Leaders Club.
Baada ya mchezo, timu ya Bongo Movie iliondoka mapema uwanjani hapo tofauti na awali kwani mara kadhaa huwa wanadumu uwanjani hapo kwa vinywaji na vitafunwa vingine.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.