Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MPYA WA ZAMBIA MICHAEL SATA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika wakati walipokutana kwenye Ofisi za Mahakama Kuu mjini Lusaka Zambia jana wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais mpya wa Zambia Michael Sata. Picha zote na Amour Nassor-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia), Mama Asha Bilal na Rais mstaafu wa Zambia Ruphia Banda, wakimsikiliza Rais mpya wa Zambia Michael Sata alipokuwa akijitambulisha kwa viongozi wakuu wa Nchi mbalimbali waliohudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwake iliyofanyika jana katika Mahakama Kuu ya Nchi hiyo mjini Lusaka Zambia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zambia Ruphia Banda kwenye ofisi za Mahakama Kuu ya Zambia wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Michael Sata zilizofanyika jana mjini Lusaka Zambia.  

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.