Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania, waishio nchini Sweden wakati alipokutana nao katika mkutano jana, katika Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden. Kushoto ni kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa Sweden, Prof. Lodhi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wenyeji wake baada ya kuwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden jana, kwa ajili ya kuzungumza na Watanzania waishio Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Watanzania, waishio nchini Sweden wakati alipokutana nao jana Septemba 25, katika Ukumbi wa Hoteli ya Gillet Clarion iliyopo Uppsala Sweden. Kuliani ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, akiwa pamoja na baadhi ya Watanzania waishio Sweden wakati Makamu wa Rais Dkt Bilal, alipokutana na kuzungumza nao jana nchini Sweden.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mrembo Miss Africa Scandnavia 2010/2011, Michelle Jeng, baada ya kumalizika kwa mkutano baina yake na Watanzania waishio nchini Sweden, uliofanyika kwenye Ukumbu wa Hoteli ya Gillet Clarion, iliyopo Uppsala nchini hapa jana Septemba 25. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Muhammed Mwinyi Mzale.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Watanzania waishio nchini Sweden, baada ya kumalizika kwa mkutano.
wakati wa maswali na majibu .......
Watanzania hao wakiuliza maswali....
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha pa kumbukumbu pamoja na baadhi ya watanzania, waishio nchini Sweden, baada ya kumaliza mazungumzo nao.
Makamu wa Rais akipokea Katiba ya Chama cha Watanzania waishio Sweden kutoka kwa Mjumbe wa Chama hicho.
No comments:
Post a Comment