Habari za Punde

*MAMA ASHA BILAL AZULU JUMBA LA MAKUMBUSHO LILILOJENGWA MIAKA ZAIDI YA 500 ILIYOPITA SWEDEN

Mama Asha Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa mambo ya kisayansi na mambo ya kale wa Chuo Kikuu cha Uppsala, Mikael Norrby, kuhusu Viumbe vilivyokaushwa na  kuhifadhiwa  katika Jumba la makumbusho la Gustavo Adolpho nchini Sweden, wakati Mama Asha alipotembelea katika Jumba hilo na kujionea mambo mbalimbali ya kisayansi yaliyomo katika Jumba hilo juzi sept. 26. Miongoni mwa mambo ya kusisimua ndani ya jumba hilo ni pamoja na mwili wa binadamu aliyefariki miaka 500 iliyopita ambao umekaushwa na kuhifadhiwa katika jumba hilo maalu kwa ajili ya mafunzo ya kisayansi pamoja na viungo mbalimbali vya wanyama na binadamu.
Mama Asha Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Chuo cha Uppsala, Mikael Norrby, kuhusu Mamba aliyekaushwa.
 Jumba la Makumbusho lililojengwa miaka 500 iliyopita nchini Sweden.
 Huyu mdada pia ni miongoni mwa maajabu yaliyomo ndani ya jumba hilo, ama kwa hakika ukimuona tu unaweza kuhisi yu hai na anakusikia na kukuona jambo ambalo wengi wamekuwa hawaamini na kujaribu kumpitishia mkono usoni mwake ili kuona kama anaweza fumba macho ama kuminya kope lakini wapi ni ametulia kama hivi hivi anavyoonekana ni Binadam aliyekaushwa miaka mingi iliyopita na kuwekwa eneo hili kama sanamu ikiwa ni maalum kwa kutoa saini ya Kaburi lililo mbele yake na pembeni yake ambalo ni la mmoja kati ya waflame waliowahi kuwapo nchini hapa.
 Haya maandishi mbele yake ni Kaburi la aliyefariki 1515.
Hili pia ni Kanisa lililopo eneo hilo la makumbusho ambalo pia ni la maajabu lukuki likiwa na makaburi mengi ndani yake ambayo kila moja limewekewa alama na jina la mtu aliyezikwa kulingana na umaarufu wake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.