Habari za Punde

*DEREVA WA ROLI AHUKUMIWA AKIWA KITANDANI CHINI YA ULINZI

Wakili huyo alidai kuwa dereva huyo akiwa na gari aina ya fuso zenye namba T582 AJF aliendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na kusababisha majeruhi 43 ambao mpaka sasa hali zao ni mbaya na kwamba mshtakiwa huyo alitumia gari hilo kinyume na aliyopewa .

Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo, Mteite alisema mahakama imepokea makosa yote aliyosomewa mshitakiwa 44 .

Hata hivyo mshitakiwa aliomba mahakama impe dhamana kutokana na hali yake kuwa mbaya kiafya, ambapo hata hivyo wakili wa serikali alimwomba Hakimu wa mahakama kuwa masharti ya dhamana yaangaliwe kwanza na yawe magumu kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya.

Aidha Hakimu huyo alimtaka mshitakiwa kuwa na fedha taslimu sh. Milion 5 na wadhamini wawili wenye nyumba ili aweze kupata dhamana.

Hata hivyo Wakili wa serikali alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuwa tarehe ya shauri hilo itakuwa Octobar mwaka huu.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.