Habari za Punde

*HATA BONGO INAWEZEKANA TUKIAMUA

 Haya ni miongoni mwa magari yanayouzwa katika Kampuni ya kuuza magari ya BMW nchini Uingereza ukiona waweza hisi ni kijigari cha watoto lakini la hasha ni gali lenye uwezo wa kuendeshwa na mtu mzima...
 Hii ni njia ya kuingia katika Steshei ya Treni ya Umeme ya Under Ground, huko chini utakuta Conection zote za mahala unapohitaji kwenda huku baadhi ya vijibao vikikuelekeza muda unaotakiwa kupanda treni yako ya mahala unapoelekea.....
 Hiki ni moja kati ya vituo vya mabasi ya kuchukua abiria 'Town Trip', vituo hivi huwa vimeipa mgongo barabara na kila kituo huwa na mashine ya kukatia tiketi ambayo hutakiwa kumuonyesha dereva pindi tu unapopanda basi kama hutokuwa na Kadi ya kusafiria 'Oyster' ambayo hukatwa kwa muda wa wiki kwa Paund 40 ama paund 20 kwa safari za njia zote ambapo waweza kupanda mabasi ya njia zote ama treni za njia zote iwapo bado kadi hiyo itakuwa na paund za kutosha. Lakini kadi ya oyster iliyokatwa kwa wiki inatumika kwa usafiri wa Treni na mabasi kwa njia zote na haijalishi umesafiri mara ngapi kwa siku....
 Hili ni moja ya duka kubwa nchini Uingereza linalouza vitu vyake kwa bei nafuu kuliko maduka yote, ambalo rai wengi wa kigeni kutoka nchi mbalimbali wanaofika nchini humo hufanya 'shooping' katika duka hili lililopo mtaa wa Oxford.
Usafiri huu hata watalii wanaofika nchini humo wakihitaji kufika katika maeneo ya makumbusho wengine hutumia usafiri huu wa bei nafuu kuliko usafiri wa aina yeyote na huzungushwa katika maeneo yote wanayohitaji.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.