Habari za Punde

*JAMBAZI SUGU LAKAMATWA IRINGA LAONYESHA LINAKOFUKIA MALI ZA WIZI BAADA YA KUIBA

  Wananchi wa Manispaa ya Iringa eneo la Mawelewele wakishuhudia mali za wizi zikifukuliwa nje ya nyumba ya Jambazi sugu baada ya kubaini nyumba ya jambazi huyo sugu aliyekuwa akifanya mauaji na kupora mali za watu eneo la Donbosco mkoani Iringa. Tukio hilo limetokea jana. Picha na Francis Godwin, Iringa

 Hizi ni sehemu tu ya mali za jambazi hilo zilizokuwa zimefukiwa katika maeneo yanayoizunguka nyumba hiyo kwa nje baada ya kufukuliwa.
Hapa si gulioni wala sokoni ama dukani bali ni nyumbani kwa Kaka Jambazi na hizi ndiyo mali za wizi alizokuwa akiiba na kuzificha kwa staili ya aina yake kwa kuzifukia nje ya nyumba yake ardhini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.