![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9lzZdnjgayxWszgXlmRnbLi7dFNfTYwX86yaa25tR56D5r7sqXBME5GQC6pmlK8r16-5k3Cw7bHgr9zkgvT89svScpWLxZnAMX5nyyil3e6fng7NvCDOeI2iH1dkxwB2Q1yD-1g6RRmk/s400/IGP%255B1%255D.jpg)
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia mwishoni mwawiki katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.
Ni jambo la kusikitisha sana kuona vitendo hivi vinaendelea kutokea na mwisho wa siku jeshi linataka kutumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwapata wahalifu hao, mi nadhani hii njia sio sahihi, sidhani kama Jeshi la polisi wanashindwa kuwapata hawa wanaowatuma wahalifu kwenda kuwadhuru maalbino hawa.
Jambo la msingi hapa sio kutangaza dau ni kuhakikisha wale wanaowatuma ndio wanakamatwa na ninaamini jeshi la polisi likishirikiana na usalama wa Taifa inawezekana kuwakamata hawa na kuwatokomeza kabisa, usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama sio pia na kuangalia usalama wa Watanzania hawa!
Ni aibu kubwa kwa Taifa letu vitendo hivi vinavyoendelea.
Kamanda wa kanda maaluum ya kipolisi, Suleiman Kova, akizungumza na kuwapa pole wanajumuiya ya wachina waishio Tanzania jijijinDra es salaam wakati walipokwenda kuaga mwili wa marehemu Mama Han Bing alieuwawa na majambazi oktoba 11.
No comments:
Post a Comment