Habari za Punde

*SAMATA NA ULIMWENGU USO KWA USO NA MGOSI KESHO

 Mbwana Samata, akiruka kupiga 'Tiktak' wakati akiwa na timu yake ya T-P Mazembe katika moja ya mchezo wa Ligi Kuu ya Kongo hivi karibuni.
 Mbwana Samata, akiwatoka mabeki wa timu pinzani wakati wa moja ya mchezo wa Ligi Kuu ya Kongo hivi karibuni.
 Mussa Hassan Mgosi, akiwa katika moja ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara alipokuwa na timu yake ya Simba kabla ya kujiunga na Motema Pembe.
*****************************
Na Sufianimafoto
Wachezaji wa timu ya T-P Mazembe ya Rubumbashi Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu, kesho watakuwa kibaruani kumkabili Mussa Hassan Mgosi wa timu ya  DC Motema pembe, wakati timu zao zitakapokutana katika mzunguko wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Kenya uliopo Rubumbashi, huku timu hizo zikiwa na kibarua kigumu zikiwania pointi tatu muhimu ili kuweza kuwa katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi hiyo ili kutwaa ubingwa.

Timu inayooongoza Ligi hiyo ni AS Vita ikiwa na pointi 28, ambayo inafuatiwa na timu ya Mbwana Samata, T-P Mazembe yenye Pointi 27, na timu ya Mgosi, DC Motema Pembe,  ikiwa katika nafasi ya tatu huku  ikiwa na Pointi 25, A FC Lupopo inashika nafasi ya nne ikiwa na Pointi 21.

Akizungumza na Sufianimafoto kwa njia ya simu kutoka Kinshasa, Mussa Hassan Mgosi, alisema kuwa mchezo huo wa kesho utakuwa ni wa upinzani zaidi kutokana na timu hizo kuwa katika nafasi nzuri katika Ligi hiyo huku kila timu ikiwa na mashabiki wengi na kila moja ikiwa na wachezaji wa kulipwa kutoka timu za Tanzania.
Aidha Mgosi alisema kuwa anatarajia kufanya mambo makubwa katika mchezo wa kesho, ili kuweza kuweka heshima na kuonyesha umuhimu wa kuwa mchezaji wa kulipwa.
Mussa Hassan Mgosi, akiwa katika moja ya mchezo wa kimataifa na timu yake ya Taifa Stars, hivi karibuni kabla ya kujiunga na Motema pembe.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.