Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC leo (Jumapili) itapambana na timu ya Wizara ya Fedha na taasisi zake katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa TCC, Chang’ombe.
Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 4.00 asubuhi na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kudumisha ushirikiano baina ya waandishi wa habari na Wizara hiyoa (na washirika wake) na wanawaomba wadau wa michezo kufika kwa wingi kuona jinsi gani waandishi na kombaini ya Hazina wanavyoweza kusakakata kandanda.
Alisema kuwa Taswa FC itatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya ziara yao ya Tanga iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
“Tunatarajia kuwa na mechi ngumu nay a kiustaarabu, tunajua timu ya Wizara ya Fedha na taasisi zake ni nzuri kwani imeshirikisha timu nyingi kama PPF, Benki Kuu, Chuo Cha Usimamizi wa Fedha na nyinginezo,” alisema Majuto.
Alisema kuwa wao wamejiandaa vilivyo na waaamini ushindi ni asili yao na hakuna kitakacho wazuia.
No comments:
Post a Comment