Habari za Punde

*VODACOM MISS TANZANIA AAGWA KUELEKEA UINGEREZA KATIKA MASHINDANO YA DUNIA

Naibu waziri wa Uchukuzi, Eng. Dkt. Athuman Mfutakamba (Mbunge) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Vodacom Miss Tanzaia 2011, Salha Israel, tayari kuiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo ya Dunia (Miss World 2011) yaliyopangwa kufanyika London, Uingereza Novemba 6.
Mbali ya kukabidhi bendera, Naibu Waziri pia alimchangia salha Dola 1000 kwa ajili ya safari hiyo huku wafanyakazi wa wizara yake wakitoa Sh. Milioni 3.4, kwa ajili ya kumchangia mrembo huyo anayekwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo ya Dunia.
Aidha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kilikabidhi Dola 2000 kwa mrembo huyo kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Nakuala Senzia.
Senzia pia alimkabidhi, Salha, kifurushi kinachoelezea vivutio mbalimbali vya utalii na uwekezaji vya Tanzania ambavyo Salha atavitumia wakati wa kuinadi nchi akiwa katika kambini ya mashindano hayo.
Habari na Picha kwa Hisani ya kitengo cha Habari cha Miss Tanzania.

 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.