Habari za Punde

*BREAKING NEEEEWZ! STARS YAICHAPA CHAD 2-1 KWAO

Timu ya Taifa Taifa Stars, inaongoza kwa mabao 2-1 katika mcheo wao dhidi ya chad, bao la kwanza limefungwa na Mrisho Ngassa katika dakika ya 11, na bao hilo lilisawazishwa na chad katika dakika ya 12 kipindi hicho hicho cha kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo kupitia mchezaji wake, Makahati Labo.

Dakika ya 80 Kipindi cha pili Shomari Kapombe aliondosha mpira katika hatari na dakika 2 baadaye yaani dakika ya 82, Nurdin Bakari aliipatia Stars bao la pili kufuatia pasi nzuri kutoka kwa Thomas Ulimwengu aliyeingia akitokea Benchi kipindi cha pili baada ya kuchukua nafasi ya Nizar Khlfan.

Kwa matokeo hayo sasa Stars itakuwa na mchezo wa marudiano na timu hiyo Novemba 15 katika Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, ambapo pia inahitajika dua za watanzania ili kuweza kupenya kuepuka kukaa benchi kwa miaka miwili ijayo iwapo tukifanya vibaya. Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki wachezaji wa Stars, Ameen

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.