
Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Ujenzi Martin Ntemo, sherehe hizo zitafanyika tarehe 12 Novemba, 2011 katika eneo la Veyula nje kidogo ya mkoa wa Dodoma saa 8 mchana.
Ntemo amesema kuwa utekelezaji wa ujenzi huo ambao ni sehemu ya barabara inayounganisha makao makuu ya Dodoma, Miji ya Kondoa, Babati, Arusha na nchi jirani za Kenya tayari umeanza.
Hii ni moja wapo ya utekelezaji wa ahadi za serikali kwa wananchi wake katika kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa zao kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
No comments:
Post a Comment